Worldreader wins the US Library of Congress 2023 Literacy Award ➤ https://bit.ly/4825npJ

Ilani ya Faragha ya Programu za Worldreader

Toleo kamili

Ilani hii ya Faragha inatawala matumizi ya programu za vifaa vya mkononi kama vile simu na tableti ambavyo vimetengenezwa na Worldreader (“Programu za Worldreader”). Programu hizi za Worldreader zimewezesha kufanya kazi kwenye simu na zinawezesha watumiaji kufikia na kusoma matini yaliyokatika haki miliki na ile wazi kwenye programu za Worldreader.

Ilani hii  ya Faragha inatumika kwenye Programu za Worldreader pekee. Iwapo kiunganishi kitakuongoza kwenye tovuti nyingine, tafadhali tazama taarifa zilizopo ili kufahamu jinsi taarifa za kulinda data yako binafsi zinavyoshughulikiwa.

1. Mdhibiti ata

Shirika linalohusika na kukusanya, kuchakatua na kutumia data binafsi zinazokuhusu (Mtawala) kutokana na maelezo ya Taratibu za Ujumla wa Ulinzi wa Data, za Umoja wa Ulaya kudhibiti ulinzi wa data, GDPR, ni:

Worldreader.org
Calle Mallorca, 318 3º 1º
08037, Barcelona, Spain
privacy@worldreader.org

Worldreader  ni shirika la kimataifa. Ilani yetu ya Faragha inaonyesha viwango vilivyowekwa na GDPR na wote wanaojihusisha na Worldreader wanafuata Ilani  hii. Watumiaji wote wanastahili data zao zilindwe na waelewe ni jinsi gani zinatumika. Tafadhali wasiliana na Mtawala kama una maswali kuhusiana na Ilani hii ya Data Binafsi, au jinsi ya  kupata haki zako kama mwenye  data.

2. Ukusanyaji, uchakatuaji na matumizi ya data binafsi

2.1  Data binafsi

“Data Binafsi” inamaanisha taarifa yoyote ya mtu anayetambulika au inayomtambulisha mtu; mtu anayetambulika ni yule anayetambulika moja kwa moja au vinginevyo, kwa kurejelea kitambulisho kama jina, namba ya kitambulisho, data kuhusu eneo alilopo, kitambulishi cha mtandaoni au kwa njia moja au zaidi mahususi kimwili, kisaikolojia, kiakili, kiuchumi, kitamaduni au kitambulisho cha kijjamii cha mtu.

Worldreader inachakatua tu data binafsi zinazokuhusu tu (mfano barua pepe, data binafsi kwenye Programu za Worldreader) kwa mujibu wa vifungu vya sheria ya ulinzi wa data. Vifungu vifuatavyo vinakutaarifu kuhusu asili, wigo na kusudi la kukusanya, kuchakatua na kutumia data binafsi.

2.2  Taarifa tunazokusanya

Ni wazi kuwa ili kukusaidia kusoma zaidi  tunahitaji taarifa kukuhusu wewe pamoja na kifaa chako. Tunakusanya taarifa hizi kadri unavyotumia huduma zetu, kwa mfano taarifa za uingiaji mtandaoni, barua pepe pamoja na taarifa nyinginezo kutoka kwa mitandao yako ya kijamii.  zaidi tazama maelezo yafuatayo.  

2.2.1 Taarifa zinazokusanywa unapotumia huduma zetu

Unapotumia huduma zetu, tunakusanya taarifa kuhusu vipengele vipi ulivitumia, namna ulivyovitumia na vifaa ulivyotumia kufikia huduma zetu.

Taarifa za utumiaji

Tunakusanya taarifa kuhusu shughuli zako kwenye huduma zetu, kwa mfano namna unavyozitumia (mfano muda na tarehe ya kuingia, vipengele unavyovitumia, vitafutio ulivyobonyeza na kurasa ulizoonyeshwa, tunarejea anwani za kurasa za wavuti, mapendekezo na matangazo uliyofungua). Zaidi ya hayo, Programu za Worldreader hukusanya taarifa kuhusu anwani  za vitabu ulivyosoma, muda uliochukua kusoma, vitafutio na taarifa nyingine kuhusu unavyosoma unapotumia Programu za Worldreader. Hii hutusaidia kuelewa ni maudhui gani yanaubora zaidi kwenye Programu za Worldreader na kupata mafunzo kuhusu usomaji wa njia ya simu. 

Taarifa za kifaa

Tunakusanya taarifa kutoka kwa na kuhusu vifaa unavyotumia kufikia huduma zetu, ikiwemo:

  • Taarifa za vifaa na programu  kama anwani ya IP, kitambulisho cha kifaa na aina, mipangilio maalumu ya kifaa na programu na tabia, mashambulio ya programu, aina ya kivinjari, toleo na lugha, mfumo wa uendeshaji, majira ya saa, vitambulisho vinavyohusiana na kuki au teknolojia zingine ambazo zinaweza kutambulisha kipekee kifaa au kivinjari; na
  • Taarifa kuhusu mtandao wa waya na simu ya rununu, kama mtoa huduma hiyo kwako na nguvu ya kimtandao (signal).

Programu za Worldreader hazikusanyi taarifa mahususi kuhusu eneo kifaa chako cha simu kilipo. Tunakusanya tu taarifa katika ngazi ya kitaifa kulingana na anwani yako ya IP. Tunafanya hivi kulingana na:

  • Kifungu 6(1)(b) cha GDPR:
    • Kwa kuzingatia majukumu ya makubaliano yetu katika sheria na masharti ya Programu za Worldreader,
    • Kwa sababu wachapishaji wetu wanaturuhusu tu kuonyesha vitabu vyao kwenye baadhi ya nchi. Kwa hivyo bila kufuatilia IP yako, hatutaweza kutambua unajiunga kutokea wapi na hivyo kushindwa kukupatia uwezo wakufikia vitabu; na
  • Kifungu 6(1)(f)cha GDPR, kufuata dhamira zetu halali.

2.2.2 Taarifa unazotupa

Unachagua kutupa taarifa fulani unaposajili akaunti kwenye moja ya huduma zetu. Ikiwemo:

  • Jina la mtumiaji;
  • Anwani ya barua pepe;
  • Nywila;
  • Jinsia;
  • Umri; na
  • Lugha uipendeleayo.

Taarifa hizi binafsi zinarekodiwa kwa misingi inayokubaliana na kifungu 6(1)(a) cha GDPR na kinatumika kubinafsisha Programu za Worldreader, kukupa uzoefu bora zaidi, na kuendelea kuboresha Programu za Worldreader na programu za kusoma kiujumla. Data hii haiwekwi wazi kwa wengine. Kama unatumia Programu ya Booksmart+, Worldreader inaweza kukusanya data kuhusu:

  • Watoto wangapi unawasomea;
  • Una uhusiano gani nao;
  • Umri wa watoto unaowasomea; na
  • Ikiwa unawasomea wavulana au wasichana.

Data hizi binafsi zinarekodiwa kwa misingi inayokubaliana na kifungu 6(1)(a) cha GDPR na kinatumika kubinafsisha Programu ya Booksmart+, kukupa uzoefu bora zaidi kwa kukupendekezea vitabu kulingana na mapendeleo na umri wa watoto wako na kuendelea kuboresha Programu za Worldreader na programu za kusoma kiujumla. 

2.2.3 Data zinazotolewa na wengine

Utaweza kutumia taarifa zako za Facebook au Google kufikia akaunti ya Programu za Worldreader. Hii inakuokoa na kukumbuka kila jina la utumiaji na nywila na inakuruhusu kushiriki vitabu na maendeleo yako kwenye mitandao ya kijamii. Tafadhali rejelea  Sera za Faragha za mitandao hii ili kuelewa jinsi inavyosimamia na kushirikisha data yako.

3. Kushiriki yako data na wengine

Tunatumia watumiaji wengine kutusaidia kuendesha na kuboresha huduma zetu. Hawa wengine wanatusaidia na shughuli mbalimbali, ikiwemo kuhifadhi data na matengenezo, uchambuzi na ulinzi wa shughuli. Worldreader haiwezi kuuza, kukodisha au kufanya biashara na taarifa hizi kwa wengineo. Worldreader itaendelea kuwa mtawala wa data yako na watoa huduma watakuwa wachakatuaji wa data yako ambao watatenda kulingana na maagizo yetu. Tunasaini makubaliano na mashirika yote tunayoshiriki data nayo kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni za data zinazotumika. Hawa watoa huduma hawataruhusiwa kutumia data yako kwa madhumuni ya kibiashara au kuweka wazi data zako kwa wengineo bila idhini yetu.

Mara kwa mara, tunaweza kushiriki data na mashirika tunayoshirikiana nayo ili kutusaidia kutekeleza programu zetu kwenye nchi mbalimbali tunazofanya kazi. Hawa washirika watatakiwa kukubaliana na Ilani hii ya Faragha na utaombwa kutoa idhini kama tutataka kushirikisha data yako binafsi. Data iliyokusanywa itapitishwa mara kwa mara kwenda kwa watoa huduma wa nje na washirika, taasisi za utafiti, washirika wanaosaidia katika kutekeleza programu zetu na wachapishaji kuboresha uzoefu wa mtumijai na kupata kujifunza kuhusu usomaji wa kidijitali. Data tu za matumizi ndizo zitakazoshirikishwa kwa washiriki. Hatutashirikisha data yako binafsi nao. Tunaweza mara kwa mara kuchapisha data tuliyokusanya kuhusu matumizai ya Programu za Worldreader na kutengeneza ripoti na masomo kutokana na data hiyo.

Tunaweza tukafichua data zako binafsi:

  • Kama inavyotakiwa kisheria, ili kuzingatia notisi, au mchakato sawa wa kisheria;
  • Tunapoamini kuwa kwa imani nzuri kuwa kufichua ni muhimu kulinda haki zetu, kulinda usalama wako na usalama wa wengine, kuchunguza udanganyifu, au kujibu ombi la serikali; na
  • Na kwa watoaji huduma wetu tunaowaamini wanaofanya kazi kwa niaba yetu,hawana matumizi huru ya taarifa tunazofichua kwao, na wamekubali kuzingatia kanuni zilizowekwa na Ilani hii ya Faragha.

Ikiwa Worldreader itajihusisha na unganisho, upatikanaji, au uuzaji wa sehemu au mali zetu zote,utajulishwa kwa njia ya barua pepe na/au notisi kwenye wavuti wetu kuhusu mabadiliko ya umiliki au matumizi ya data binafsi, vilevile maamusi unayoweza fanya kuhusu data yako binafsi.

4. Uhamishaji wa data nje ya Eneo la Uchumi wa Ulaya (EEA)

Ushirikishwaji wa data binafsi kama zilivyoelezwa kwenye vipengele vilivyopita, wakati mwingine unahusisha kuhamisha data kati ya mipaka mbalimbali. Kwa mfano, pale ambapo Programu za Worldreader zinapatikana kwa watumiaji walioko ndani ya Eneo la Uchumi wa Ulaya (“EEA”), data yao binafsi inaweza kusafirishwa kwenda Marekani au tawala nyinginezo. Tunatumia kanuni za viwango vilivyoidhinishwa na Tume ya Ulaya (EC) au ulinzi unaofaa kuruhusu kuhamisha data kutoka Eneo la Uchumi wa Ulaya kwenda nchi zingine. Vifungu maalumu vya mikataba ni kujitolea kati ya makampuni yanayohamisha data binafsi, inayowafunga kulinda faragha na usalama wa data yako binafsi kuhakikisha kuwa viwango vya ulinzi vilivyohakikishiwa na GDPR vinafuatwa.

5. Watoto

Hatutumii Programu za Worldreader ili kupata data binafsi kwa kujua kutoka kwa au kuuza kwa watoto chini ya miaka 16. Ikiwa mzazi au mlezi atajua kuwa mtoto wake ametupatia data binafsi bila idhini, anaweza kuwasiliana nasi kupitia privacy@worldreader.org. Tutafuta taarifa hizo kwenye mafaili yetu kwa wakati unaofaa.

6. Sera ya kutunza data, kusimamia taarifa zako

Tutatunza data iliyotolewa na mtumiaji kwa kipindi chote utakachotumia Programu za Worldreader na kwa muda unaofaa baadaye. Tutatunza kiotomatiki taarifa zilizokusanywa kwa muda wa miaka 10. Tunaweza tunza data iliyokusanywa na iisiyojulikana kwa muda usiojulikana kwa madhumuni ya utafiti.

7. Ulinzi

Tunajali kuhusu kulinda usiri wa data yako binafsi. Tunatoa ulinzi wa kielektroniki na utaratibu wa kulinda data binafsi na kuidumisha. Kwa mfano, tunadhibiti ufikiwaji wa taarifa hizi kuwa kwa waajiriwa walioidhinishwa na wanakandarasi wanaohitaji kujua taarifa hizi ili kuendesha, kutengeneza au kuboresha Programu za Worldreader. Tafadhali jua kuwa, ingawa tunataka kutoa usalama unaofaa kwenye taarifa tunazochakatua na kudumisha, hakuna mfumo wa usalama unaoweza kuzuia uvamizi wa kimtandao kikamilifu.

8. Haki zako

Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia taarifa za mawasiliano yetu kwenye kipengele 1 hapo juu wakati wowote kama una maswali kuhusiana na haki zako au mada zinazohusiana na data binafsi. Una haki zifuatazo:

8.1 Haki ya kufikia taarifa

Una haki ya kuomba,  na bila malipo wakati wowote aarifa kuhusu data binafsi inayokuhusu  na iliyohifadhiwa na Worldreader, asili na wapokeaji wa data hizi, madhumuni ya kuchakatua data hiyo, muda uliopangwa wa kuhifadhi data na nakala ya data binafsi inayochakatuliwa (Kifungu 15 cha GDPR).

8.2 Haki ya marekebisho

Pia una haki ya kupata bila kuchelewa marekebisho ya data binafsi isiyo sahihi na  kukamilisha  data binafsi isiyokamili (kifungu 16 cha GDPR).

8.3 Haki ya kuondoa idhini

Una haki ya kuondoa idhini, bila kutaja sababu, na idhini ya kuchakatua data wakati wowote. Hii haitadhuru sheria za kuchakatua kulingana na idhini yako ya mwanzo kabla ya kuondoa (Kifungu 7(3) cha GDPR).

8.4 Haki ya kufuta

Una haki ya kutaka kufutwa kwa data yako binafsi inayokuhusu bila kucheleweshwa kusikostahili kama data binafsi si muhimu kuhusiana na madhumuni iliyokusanyiwa au kuchakatwa  au kama utaondoa idhini ya  mchakato halali na hakuna misingi ya kisheria ya kuchakatua data hiyo. Kama unapinga uchakatuaji wa data na hakuna msingi unaopingana naokisheria kuhusu uchakatuaji, data yako binafsi itafutwa. Hatimaye, data yako binafsi itafutwa kama uchakatuaji si wa kisheria kulingana na sababu za kisheria (Kifungu 17 cha GDPR).

8.5 Haki ya kuzuia uchakatuaji

Una haki ya kuzuia uchakatuaji kama unapinga usahihi wa data binafsi kwa muda unaokuwezesha kupitia usahihi wake. Uchakatuaji wa data unazuiwa kama uchakatuaji huo si wa kisheria na unakinzana na ufutaji wa data binafsi na kisha kuomba kuzuia uchakatuaji, au kama hatuhitaji tena data binafsi kwa madhumuni husika, ila tunahitaji kwa ajili ya kuweka, au kujenga madai ya kisheria, au kama umewahi kupanga uchakatuaji, unasubiria udhibitisho huenda Worldreader ina misingi ya kisheria ya kutunza data binafsi inayokinzana na matakwa yako (kifungu 18 cha GDPR).

8.6 Haki ya uhamishaji data

Una haki ya kupokea data binafsi inayokuhusu na uliyotupatia, kwa muundo unaotumika kwa kawaida  na ulio katika mfumo unaosomeka na mashine na una haki ya kusambaza data hiyo kwenda kwa mtawala pale ambapo uchakatuaji unafanyika kwa idhini au mkataba wa data binafsi inayochakatwa kiotomatiki (Kifungu 20 cha GDPR).

8.7 Haki ya kupinga

Hatimaye ,una haki ya kupinga wakati wowote uchakatuaji wa data binafsi inayokuhusu katika siku za usoni. Una haki ya kupinga wakati wowote mkusanyiko wa maumbo ya watumiaji na uchakatuaji wa data binafsi inayoendana na inayokuhusu pale ambapo uchakatuaji unafanyika kwa misingi ya dhamira halali. Data binafsi inayokuhusu haitachakatuliwa pale ambapo hakutakuwa na misingi halali ya kuichakatua na ikiwa inapita matakwa yako, haki na uhuru (kifungu 21cha GDPR).

8.8 Haki ya kuwasilisha malalamiko

Kwa kuongezea, una haki ya kuwasilisha malalamiko yako kwa msimamizi mamlaka (Kifungu 77 cha GDPR).

9. Mabadiliko

Ilani ya Faragha inaweza kusasishwa mara kwa mara kuonyesha mabadiliko kwa mazoea yetu ya faragha na tutachapisha toleo la sasa katika wavuti yetu na ndani ya Programu za Worldreader ambazo unatumia. Ikiwa mabadiliko haya yana umuhimu, tutaarifu watumiaji kupitia arifa za Programu za Worldreader. Tunakukuhimiza kuweka upendeleo wako wa Programu za Worldreader ili kupokea arafa hizi na / au kukagua Ilani ya Faragha ya hivi karibuni kuhusu kaida  zetu za faragha.

 

Sasisho la mwisho: Machi 2020